
Aliyekuwa Mgombea wa Urais nchini Kenya kupitia Azimio la Umoja, Raila Odinga amesema Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) Wafula Chebukati anapaswa kujiondoa kwenye uchaguzi wa Ugavana, Mombasa na Kakamega ili haki iweze kutendeka huku akibainisha kuwa Naibu wa Chebukati, Juliana Cherera ndiye anafaa kusimamia chaguzi hizo mbili.
