Back to top

Ofisi za Msajili wa Vyama kukamilika baada ya miezi 12

23 June 2022
Share

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,Bunge na Uratibu) Bw.Kaspar Mmuya amepongeza maendeleo ya ujenzi wa ofisi ya msajili wa vyama vya siasa nchini zinazojengwa eneo la Kilimani Jijini Dodoma zitakazogharimu zaidi ya shilingi bilioni 20 huku akibainisha kuwa ujenzi huo unatarajiwa kukamilika baada ya miezi 12 na akasisitiza kuongezwa kwa rasilimali watu, muda wa kazi pamoja na vifaa ili kufanya kazi ndani ya muda uliopangwa.
.
Aidha, Bw.Mmuya amemuagiza mshauri wa ujenzi kufika mara kwa mara katika eneo la mradi na kufanya kazi kwa kushirikiana na watendaji wengine kufahamu hali ya ujenzi na kutatua changamoto pindi zinapojitokeza kuhakikisha jengo linajengwa katika hali ya uimara, ubora na usalama.

Nimshauri mtaalamu wetu awe anatembelea mara kwa mara jengo hili kujionea maendeleo ya kazi kama kuna shida yoyote inatatuliwa  kwa wakati na kufanya marekebisho yanayaotakiwa,”alisisitiza.