Back to top

Ole Gunnar Solskjaer ana imani na Jadon Sancho

22 September 2021
Share

Kocha wa Man United, Ole Gunnar Solskjaer amesema anaamini kuwa winga wake mpya wa timu hiyo, Jadon Sancho atakuwa mshambuliaji mahiri wa Man United miaka kadhaa ijayo.

Sancho aliyejiunga na United akitokea Borrusia Dortmund ameshindwa kuonyesha makali yake ndani ya uwanja ingawa mashabiki wa Man United wanaamini kuwa anatakiwa kupewa muda na huko mbele atafanya vizuri.

Kocha huyo wa United amesema anaamini kuhusu uwezo wa kinda huyo na hana shaka kuwa anaweza kuwa staa wa United miaka mingi ijayo.