Back to top

Operesheni ya Polisi Dar, silaha na wahalifu wakamatwa.

08 June 2021
Share

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, amesema kufuatia Operesheni ya wiki moja iliyofanyika katika Jiji la Dar es salaam, wamefanikiwa kukamata silaha za moto pamoja na wahalifu waliokuwa wakijihusisha katika matukio mbalimbali ya kihalifu.
.
IGP Sirro amesema hayo leo wakati wa kikao kazi cha kufanya tathmini, mafanikio na changamoto ambapo pia ameelekeza kufanyika kwa operesheni ya mwezi mmoja kwa nchi nzima ili kubaini mianya ya uhalifu na wahalifu.
.
Aidha, IGP Sirro amewaelekeza Makamanda wa Polisi nchini kufanya operesheni ya usalama barabarani dhidi ya magari yote yasiyokidhi vigezo vya kuwepo barabarani ili kuwahakikishia usalama watumiaji wa vyombo vya moto.