
Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhandisi Cyprian Luhemeja, ameuagiza Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA), kuhakikisha hadi kufikia Juni 2024, uwe umesajili maeneo yote ya kazi nchini pamoja na kuhakikisha kwamba maeneo hayo yanapatiwa miongozo ya namna ya kuwalinda wafanyakazi dhidi ya vihatarishi vya magonjwa na ajali.
.
Katibu Mkuu huyo ametoa maagizo hayo wakati akizindua Baraza la Tano la Wafanyakazi wa OSHA, Jijini Arusha, ambapo amebainisha kuwa OSHA imepewa dhamana ya kujenga nguvukazi salama na yenye afya njema kwa maendeleo endelevu ya Taifa, hivyo ni lazima Taasisi hiyo itimiza wajibu huo ipasavyo.
.
Aidha, akizungumza baada ya uzinduzi wa baraza hilo, Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi. Khadija Mwenda, amesema Taasisi yake imeyapokea maagizo ya Katibu Mkuu na kwamba itayatekeleza ipasavyo.
