Back to top

PACQUIAO NA MAYWEATHER KUZICHAPA TENA SEPTEMBA 2026

24 February 2026
Share

Wanandondi maarufu Manny Pacquiao na Floyd Mayweather wamekubaliana kuzichapa tena katika pambano la kitaalamu mnamo mwezi Septemba.

Pacquiao, (47) na Mayweather, (48) watapigana Sphere huko Las Vegas Jumamosi, Septemba 19, huku pambano hilo likionyeshwa moja kwa moja kwenye Netflix.

Itakuwa pambano la kwanza la kitaalamu kwa Mmarekani huyo tangu amshinde Conor McGregor raundi ya 10 ya pigano kwa ‘knockout’ tangu mwaka 2017.

Pacquiao wa Ufilipino alistaafu kutoka kwenye mchezo huo ili kujikita zaidi kwenye taaluma yake ya kisiasa mwaka wa 2021 lakini alirudi ulingoni Julai iliyopita kupambana na bingwa wa WBC wa uzito wa welterweight Mario Barrios, ambaye alihifadhi taji lake baada ya kutoka sare.

Mayweather na Pacquiao walikutana kwa mara ya kwanza mwaka wa 2015, katika kile kilichoitwa 'Pambano la Karne' na linasalia kuwa la kihistoria katika ndondi.

Mayweather aliibuka na ushindi, akimshinda Pacquiao kupitia uamuzi mpana wa pamoja huko Las Vegas.

Pacquiao, mshindi wa mataji 12 ya dunia katika madaraja manane ya uzito, alisema: "Mimi na Floyd tuliipa dunia pambano kubwa zaidi katika historia ya ndondi."