Zaidi ya hekta 500 za mazao ya Mahindi na Mpunga katika tarafa za Mng'eta na Mlimba wilayani Kilombero zimeharibiwa vibaya na Panya walioibuka na kuvamia mazao hayo yaliyopandwa shambani jambo lililosababisha hofu kubwa kwa wakulima kukosa mazao ya chakula na biashara kwa msimu wa kilimo mwaka 2017-18 licha ya serikali kupambana vikali kuwatokomeza Panya hao waharibifu.
Akizungumza katika kikao cha baraza la Madiwani katibu tawala wilaya ya Kilombero Robert Selasela kwa niaba ya mkuu wa wilaya hiyo James Ihunyo amesema licha ya panya hao kuwa tishio serikali imejitahidi ili kuona shuhuli za Kilimo zinaendelea.
Kwaupande wake mwenyekiti wa halmashauri hiyo bwana David Lugazio amesema pamoja na changamoto hiyo lakini katika elimu halmashauri imejitahidi kuhakikisha elimu inasonga mbele na kufanikiwa kupiga hatua kutoka nafasi 18 ya ufaulu hadi kufikia nafasi ya 11 jambo lilil pongezwa na katibu tawala wa mkoa wa Morogoro Cliford Tandari na kuwapa vyeti walimu waliofanya vizuri katika shule zao.