Back to top

Papa Francis awataka wakristo kutovunjika moyo kipindi hiki cha Corona

04 April 2021
Share

Mamilioni ya waumini wa dini ya Kikristo duniani wanashehekea leo sikukuu ya Pasaka chini ya vizuizi vikali vya kukabiliana na virusi vya Corona ambavyo maambukizi yake bado yanaongezeka kwenye mataifa mengi ulimwenguni.

Katika ujumbe wake alioutoa kwenye misa ya mkesha wa Pasaka kukumbuka kufufuka kwa Yesu Kristo, kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis ametoa wito kwa waumini kutovunjika moyo hata katika kipindi kigumu cha janga la Corona.

Kwa mwaka wa pili mfulilizo makao makuu ya Kanisa Katoliki Duniani Mjini Vatican yamelazimika kupunguza matukio ya kidini yanayoambatana na shehere za pasaka ili kuondoa uwezekano wa kusambaa virusi vya Corona.

Baadaye leo Papa Francis anatarajiwa kuongoza misa ya Pasaka itakayohudhuriwa na idadi ndogo ya watu kwenye kanisa la Mtakatifu Petro mjini Vatican.