Back to top

Parachichi kuwa zao la biashara na mbadala wa zao la kahawa Mbinga.

06 January 2020
Share

Halmashauri ya mji wa Mbinga mkoani Ruvuma pamoja na kuimarisha mazao mengine imelifanya zao la parachichi  kuwa la biashara na mbadala wa zao la kahawa pindi soko lake linapoyumba.

Baada ya kuona fursa kwenye zao la parachichi Mkuu wa idara ya kilimo, umwagiliaji na ushirika wa halmashauri hiyo Dkt Kesam Maswaga amewataka wakulima kuchangamkia fursa ya kulima zao hilo.

Kwa upande wao wakulima katika halmashauri ya mji wa Mbinga wamesema pamoja na kulima  mazao mengine kama maharage pia wanalima zao hilo na mafanikio yake yameanza kuonekana na wamefanikiwa kuboresha maisha yao.