Back to top

PARIS VITANI NA KUNGUNI KUELEKEA OLIMPIKI 2024

04 October 2023
Share

Wakati Paris ikijiandaa kukaribisha wageni nusu milioni, wanaotarajiwa kuwasili wakati wa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya joto ya 2024, kuna ugeni (kunguni) ulioibuka bila mualiko ambao wanapambana ili kuwaondoa.

Serikali ya Ufaransa wiki iliyopita, ilitangaza kuwa wanazindua juhudi za pamoja za kupambana na kunguni, ambao wamejitokeza kwa wingi katika usafiri wa umma, sinema na hospitali.

Wadudu hao wanaonyonya damu, wameonekana katika maeneo mbalimbali ikiwemo kwenye treni za mwendo kasi, na katika uwanja wa ndege wa Charles de Gaulle mjini Paris, huku wasafiri waliochukizwa wakichapisha video kwenye mitandao ya kijamii.