
Magari 10 na piki piki 27 vimekamatwa na jeshi la polisi mjini Bujumbura nchini Burundi.Msemaji wa wizara ya usalama wa raia anafahamisha kwamba magari hayo ambao ni mapya,yalio ingia nchini mwaka 2010 yalitarajiwa kutumiwa kuvuruga uchaguzi wa kura ya maoni unaopangwa Mei 17 mwaka huyu.Magari hayo yadaiwa kwamba yaliagizwa nje ya nchi na aliekuwa kiongozi wa zamani wa chama tawala, El Hadj Hussein Radjabu.
Magari hayo na pikipiki hizo vimekamatwa mtaani Rohero mjini Bujumbura ambapo yalikuwa yamefichwa tangu mwaka 2010.
Msemaji wa Wizara ya Usalama na Kulinda majanga anasema uchunguzi umeanzishwa ili kutambuliwe wale wote wanao husika na njama hiyo ya kuvuruga uchaguzi wa kura ya maoni.