Back to top

PINDA AKABIDHI MAGARI MAWILI YA WAGONJWA

04 February 2024
Share

Mbunge wa Jimbo la Kavuu lililopo katika Halmashauri ya Mpimbwe wilayani Mlele, mkoani Katavi ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geofrey Pinda, amekabidhi magari mawili ya wagonjwa ili yasaidie kusafirisha wagonjwa wanaohitaji huduma ya dharula katika Halmashauri hiyo.
.
Akizungumza baada ya kukabidhi magari hayo, Mhe.Pinda ameitaka Halamshauri hiyo kuhakikisha magari hayo yanatunzwa vizuri na yanatumika kwa malengo yaliyokusudiwa.
.
Aidha, Mhe.Pinda amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan kwa kuimarisha huduma za afya kwenye Jimbo hilo, ikiwemo ujenzi wa vituo vya afya na zahanati.
.
Kwa mujibu wa Mbunge huyo wa Jimbo la Kavuu, wakati anaingia madarakani mwaka 2020, vituo vya afya kwenye jimbo lake vilikuwa viwili na kuvitaja kuwa ni kile cha Usevya na Mamba.
.
Hata hivyo, ameweka wazi kuwa, kwa sasa katika jimbo lake vimeanzishwa vituo vingine vitatu vya Majimoto, Kibaoni, Kasansa Pamoja na Zahanati ya Mwamapuli inayokwenda kuanza kazi.
.
Amesema, ataendelea na juhudi mbalimbali za kuimarisha huduma za sekta ya afya katika jimbo la Kavuu kwa kuwa afya ni muhimu huku akiwaahidi wananchi wa jimbo lake kupambana kwa hali na mali ili jimbo hilo libadilike kimaendeleo na pale atakapomaliza muda wake aache alama itakayomfanya aendelee kukumbukwa.
.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mpimbwe Shamimu Mwariko amesema, jukumu la halmashauri yake ni kuhakikisha magari waliyokabidhiwa yanaenda kusaidia na kuboresha huduma za afya kwa wananchi wa Mpimbwe.