Back to top

PINDA ATAKA MAENEO YA UMMA KULINDWA NA MABANGO

21 July 2023
Share

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Geophrey Pinda, amezitaka ofisi zote za umma na Taasisi za Serikali kulinda maeneo yao kwa mabango yanayoonekana ili kuepuka kuvamiwa na wananchi wanaozunguka maeneo hayo.

Pinda ameyasema hayo wakati alipofanya ziara ya kukagua maeneo ya Taasisi zenye migogoro ya ardhi na wananchi ambapo alizuru eneo lenye mgogoro wa fidia kati ya wananchi na Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Katavi na mgogoro wa ardhi wa wananchi na Chuo cha Kilimo cha Katavi vyote vilivyopo mtaa wa Rungwa wilayani Mpanda mkoa wa Katavi.

"Tengenezeni vile vibao vya kujenga, kuvipaka rangi na kuandika kwa maandishi ya kuonekana kuwa eneo hili ni mali ya Serikali au Taasisi fulani na hairuhusiwi kufanyiwa shughuli za kibinadamu au za aina yoyote, hii itasaidia kupunguza migogoro ya ardhi na fidia zisizi za lazima"Amesema Pinda.

Ameongeza kuwa maeneo mengi hasa ya Halmashauri yamekuwa ni chanzo kikuu cha mgogoro kwa sababu hakuna mabango ya wazi ya tahadhari kwa wakazi wa karibu jambo ambalo linasabisha uvamizi unaogharimu fidia ambazo zinaweza kuzuilika kwa kuweka mabango tu.