Back to top

Pinda awataka viongozi wa dini nchini kuendelea kuliombea taifa amani.

27 September 2020
Share

Waziri Mkuu Mstafu Mhe.Mizengo Pinda amewataka viongozi wa madhehebu ya dini nchini kuendelea kuliombea taifa amani katika kipindi hiki cha kampeni za kuelekea uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani ambapo amesema amani na utulivu ni msingi wa maendeleo ya taifa na kuwasihi watanzania kujiepusha na vitendo vinavyoweza kuhatarisha uvunjifu wa amani.

Mhe.Mizengo Pinda ametoa rai hiyo jijini Dodoma mara baada aya kuzungumza na waumini ambao ni wanachama wa chama cha ushirika wa  akiba na mikopo KKKT Arusha Road ambapo amesema viongozi wa dini wana nafasi kubwa ya kuwasihi Watanzania kujiepusha na uvunjifu wa amani.

Kwa upande wake Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Dayosi ya Dodoma Amon Kinyunyu amewaomba Watanzania kuungana kwa pamoja kuendelea kuliombea taifa ili kuepusha nchi kuingia kwenye machafuko.

Naye Mwenyekiti wa bodi ya ushirika wa akiba na mikopo KKKT Arusha Road Bw.Ibrahim Sumbe amesema tangu kuanzishwa kwa ushirika huo wamekuwa wakipata hati safi ambapo tangu kuanzishwa kwa chama hicho wamekwishatoa mikopo ya zaiadi ya shilingi bilioni 14 kwa ajili ya kusaidia wananchi.