Back to top

PINGU YA NYUKI YAIBUA GUMZO UGANDA

13 January 2024
Share

Mwanamke anayetambulika kama Kuhani wa jadi huko nchini Uganda ameibua gumzo baada ya kumfunga pingu ya nyuki mwanaume mmoja aliyekamatwa kwa wizi huko Koboko.

Video iliosambaa katika mitandao ya kijamii imemuonesha mwanaume huyo, anayedaiwa  kuwa mwizi, akiwa amezingirwa na kundi la nyuki katika mikono yake wakati akipelekwa katika kituo  cha polisi.

Cha ajabu ni kwamba nyuki hao hawakuonyesha dalili ya kuruka wala kumng'ata mtuhumiwa huyo wa wizi, wala mtu yoyote aliyekuwa karibu na mwanaume huyo.

Mtuhumiwa huyo amekabidhiwa kwa Jeshi la Polisi nchini humo.