
Serikali imesema Plastic Surgery sio tu kwa ajili ya kuongeza makalio bali hutumika pia kuwapa matibabu watu waliopata majeraha makubwa ya viungo, kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ajali.
.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya, Mhe.Godwin Mollel, wakati akijibu hoja ya Mbunge wa Jimbo la Kisesa, Luhaga Mpina, aliyehoji ni kwa nini serikali inapoteza fedha kwa kuwekeza kwenye vifaa vya kuongeza makalio.
.
Akitoa ufafanuzi huo, Mhe.Mollel amesema kabla ya uwekezaji huo, Watanzania wengi walikuwa wakienda nchi za nje ikiwemo Uturuki kutafuta huduma hiyo, na walipeleka fedha nyingi kwenye nchi hizo lakini kwa sasa fedha hizo zinabaki hapa nchini na kuendelea kuimarisha sekta ya Afya.
