Back to top

Polepole aagiza kuhakikiwa upya wamiliki wa vizimba vya soko morogoro.

11 January 2021
Share

Katibu wa Itikadi,Siasa na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) taifa Bw. Hamphrey Polepole ameuagiza uongozi wa mkoa na Manispaa ya Morogoro, kuhakiki upya wafanyabiashara waliopewa vizimba ndani ya soko kuu la morogoro ili kuondoa malalamiko kwa wafanyabiashara.

Polepole ametoa agizo hilo wakati akikagua miradi ya kimkakati inayojengwa katika Manispaa ya Morogoro ikiwemo ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) soko kuu la Morogoro, pamoja na mradi wa maji wa Magadu.