
Kuelekea kufunguliwa kwa shule za msingi na sekondari nchini, Jeshi la Polisi limewataka madereva na makondakta wa daladala kuepuka vitendo vinavyoweza kuwaumiza watoto, kimwili au kisaikolojia na kuwanyima haki zao za msingi huku likibainisha kuwa limejipanga vizuri katika kusimamia sheria ili watoto waendelee kuwa salama waendapo na kurudi shuleni.