Back to top

POLISI ALIYEMJERUHI MTOTO WAKE KWA FIMBO MBARONI

23 January 2023
Share

Askari wa Jeshi la Polisi mwenye namba H 4178 PC, Abati Benedicto Nkalango, miaka 27, anashikiliwa na Jeshi hilo akidaiwa kumshambulia mtoto wake aitwaye Benedicto Abati, miaka 7, mwanafunzi wa darasa la kwanza, shule ya msingi Gappa, kwa kumshambulia na fimbo sehemu mbalimbali za mwili wake.
.
Taarifa hiyo imetolewa na Jeshi Polisi kufuatia video iliyosambaa mitandaoni ikimuonyesha mtoto huyo anayedaiwa kujeruhiwa na Askari huyo, ambaye ni Mzazi wake.