
Mtandao wa Polisi Wanawake Mkoa wa Arusha kwa kushirikiana na Dawati la Jinsia na Watoto katika kuelekea kilele cha siku 16 za kupinga ukatili, wametoa msaada wa vitu mbalimbali kwa wafungwa na mahabusu wanawake walioko katika gereza kuu Arusha.
Akikabidhi msaada huo, Mkuu wa Polisi Wilaya ya Arusha, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi SSP Georgina Matagi, kwa niaba ya Mwenyekiti wa Mtandao huo amebainisha kuwa, Jeshi la Polisi linashirikiana na makundi yote katika jamii kupinga na kukemea vitendo vya ukatili.
SSP Matagi amesema wameona ni vyema mwaka huu katika
kuadhimisha siku 16 za kupinga ukatili kwenda kuwatembelea wafungwa gerezani kwa ajili ya kuwapa moyo na hamasa ili pindi wanapomaliza vifungo vyao kuwa mabalozi wazuri wa kupinga na kukemea vitendo hivyo katika jamii.