
Jeshi la Polisi na Taasisi ya Mitambo Mizito na Teknolojia (IHET) wametengeneza mfumo uitwao Driving School Registration System(DSRS) ambao utatumika kutambua shule za udereva ambazo zimesajiliwa kwa mujibu wa sheria.
.
Akifungua mafunzo ya mfumo huo, leo Februari 19, 2024, Msimamizi Mkuu wa kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Naibu Kamishna wa Polisi, Frasser Kashai, amekipongeza Chuo cha Ufundi Arusha na kikosi cha usalama barabarani kwa ubunifu huo, ambao utawezesha kupata wataalam wa fani waliopata mafunzo katika vyuo vinavyotambuliwa na serikali.
.
Kwa upande wake Afisa Mnadhimu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, ACP Pili Misungwi, amesema mfumo huo unakwenda kudhibiti madereva wasio na sifa ambapo amewaomba Wakuu wa kikosi hicho kuyapokea mafunzo hayo ambayo yanakwenda kumaliza changamoto zilizokuwepo ikiwemo kudhibiti shule za udereva zisizokuwa na sifa hapa nchini.
