Back to top

POLISI KUIMARISHA ULINZI NA USALAMA KWA WATALII

13 July 2023
Share

Jeshi la Polisi limesema kuwa litaendelea kuunga mkono juhudi za Mhe.Rais Samia Suluhu hassan, katika kukuza utalii na kuongeza watalii nchini kwa kuimarisha ulinzi na usalama kwa watalii wa ndani na nje ya Nchi.
.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Kituo cha Utafiti cha Jeshi la Polisi, ACP Ralf Meela, katika mafunzo yaliyotolewa na wakufunzi kutoka chuo cha Taifa cha Utalii (NCT) kwa wanafunzi wanaoendelea na kozi mbalimbali katika Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam (DPA).
.
Aidha, ACP Meela, amebainisha kuwa Mafunzo hayo yanakwenda kuuongeza weledi katika kutoa huduma bora kwa wageni ambao wanafika nchini kwa ajili ya utalii.