Back to top

POLISI WAPIGA MARUFUKU MIKUTANO YA BOBI WINE

14 September 2023
Share

Polisi nchini Uganda wamepiga marufuku mikutano ya kisiasa inayoandaliwa na kiongozi wa upinzani Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine, akidaiwa kukiuka utaratibu na kumchafua Rais wa nchi hiyo.
.
Akitoa taarifa hiyo, Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi nchini humo, Tumusiime Katsigazi, amedai kuwa mtu mmoja amefariki huku wengine 10 wakijeruhiwa katika mikutano ya chama cha National Unity Platform (NUP), kinachoongozwa na Bobi Wine.
.
Hata hivyo Mwanasiasa huyo ambaye pia ni msanii wa muziki nchini humo amesema ataendelea na mikutano yake licha ya Polisi kuipiga marufuku.