Back to top

POLISI WATEKETEZA SILAHA HARAMU 6,208

22 November 2022
Share

Jeshi la Polisi limeteketeza silaha haramu 6,208, ambapo limebainisha kuwa silaha hizo ni pamoja na silaha 1,228 ambazo zilisalimishwa kwa hiari katika kampeni ya mwezi wa Afrika na Silaha 4,760 zilipatikana kutokana na Operesheni mbalimbali za Vyombo vya ulinzi na Usalama.


Zoezi hilo la uteketezaji silaha hizo limefanyika leo Novemba 22, 2022, katika viwanja vya shabaha vya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) vilivyopo Kunduchi, mkoani Dar es Salaam, likiongozwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Jumanne Sagini