Back to top

Polisi wawatawanya waandamanaji kwa mabomu ya machozi Iraq

07 November 2019
Share

Vikosi vya usalama nchini Iraq vimefyatua mabomu ya kutoa machozi na risasi za moto hewani kuwatawanya waandamanaji katika mji mkuu Baghdad huku maandamano ya kuipinga serikali yakisambaa nchini humo.

Makabiliano hayo yametokea karibu na madaraja matatu makuu ya Baghdad, ya Ahrah, Shuhada na Bab al-Muatham, ambayo yamekuwa kitovu cha maandamano.

Waandamanaji awali walikuwa wamelifunga daraja la Shuhada karibu na mto Tigris tangu jana Jumatano,huku maelfu kwa maelfu wakijiunga na maandamano mjini humo, na katika mikoa mengine ya Kusini kudai mabadiliko ya kisiasa.

Waandamanaji wanalalamika kuhusu rushwa, ukosefu wa ajira na huduma mbovu za kimsingi huku kukiwa na matatizo ya kukatika umeme kila mara.