Jeshi la Polisi mkoani Lindi, linamshikilia mfanyabiashara Elishi Magoma, mkazi wa wilaya ya Liwale, mkoani Lindi, kwa kosa la kuhamasisha vurugu na uchochezi kwa njia ya Mtandao.
Kaimu kamanda wa Polisi, mkoa wa Lindi,Renatusi Ngasa,amesema mtuhumiwa alituma sauti katika kundi la Telegram Lindi, makala fupi yenye kauli za uchochezi.