Back to top

POLISI YATAJA SABABU ZA KUPIGA MARUFUKU NAMBA ZA 3D

03 March 2024
Share

Jeshi la Polisi nchini limetaja sababu za kupiga marufuku namba za magari zilizoongezwa ukubwa (3D), ambapo limesema sababu kubwa ni kwamba hazisomeki kwa urahisi hasa nyakati za usiku kwani hazing'ai, pia hazisomeki kwa urahisi kwenye mifumo ya kielektroniki.
.
Jeshi hilo limetoa sababu hizo kupitia mitandao yake ya kijamii, ambapo limebainisha sababu zingine kuwa ni, hazitengenezwi kwa kuzingatia viwango na sheria za nchi, malighafi zinazotumika kuzitengeneza ubora wake haujathibitishwa na TBS, ni rahisi kutumiwa na wahalifu kutenda uhalifu pia zinatengenezwa na wasiotambulika kisheria.