Back to top

Pompeo ateta na viongozi wa Urusi.

15 May 2019
Share

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani Mike Pompeo amefanya mazungumzo na Rais Vladimir Putin wa Urusi pamoja na waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo Sergei Lavrov, akijaribu kutuliza wasiwasi wa kimataifa kuhusiana na kuongezeka kwa mvutano ambao unahofiwa kuweza kuzidisha mzozo kati ya Marekani na Iran.

Pompeo amesema kimsingi Marekani haitafuti vita na Iran, na kuongeza lakini kwamba nchi yake imekwishabainisha kuwa ikiwa Iran itatishia maslahi ya Marekani, kitisho hicho kitajibiwa kwa njia inayoeleweka. 

Viongozi hao wa Marekani na Urusi wamezungumzia pia masuala mengine ambayo yanazusha tofauti kubwa baina yao, ikiwemo mizozo ya Venezuela, Iran, Ukraine na Syria. 

Pompeo vile vile ameionya Urusi dhidi ya kuingilia katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2020 nchini Marekani. Kila upande umeelezea nia ya kuboresha uhusiano baina yao ambao unachechemea, na kusaka njia za kushirikiana.