Back to top

'Prof.Baregu alisimama imara kupigania mfumo wa vyama vingi'

13 June 2021
Share

Mwanazuoni maarufu Prof.Mwesiga Baregu ambaye pia aliwahi kuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) amefariki dunia.

Taarifa za kifo hicho zimethibitishwa na Katibu Mkuu wa CHADEMA Mhe.John Mnyika kwenye taarifa yake kwa umma, ambapo amesema watatoa taarifa za ziada baada ya mashauriano na familia kuhusu wa mipango ya mazishi.

Amemueleza Prof.Baregu kama mwanazuoni ambaye alisimama imara kupigania mfumo wa vyama vingi nchini, kuasisi na kuuishi wakati wote. 

                                 Marehemu Prof.Mwesiga Baregu.

Kupitia ukurasa wa Twitter, Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe ameandika:"Msiba wa Prof. Mwesiga Baregu ni mzito sana. Hakika mchango wake mkubwa katika ujenzi wa demokrasia ya nchi yetu na haswa katika mchakato wa Katiba ambayo yeye alikuwa Mjumbe wa Tume ya Katiba utakumbukwa Daima. Alikuwa Mwanazuoni wa Umma na Mhadhiri mahiri”.

Naye Waziri wa Viwanda na Biashara,  Profesa Kitila Mkumbo ameandika "Pumzika kwa amani Profesa Baregu. Mmoja wa wasomi walioamini kuwa huwezi kutenganisha taaluma na siasa. Ulitufundisha baadhi yetu tunaokubali msimamo huo wasomi wanaweza kufanya siasa bila kupoteza sifa zao”.