Back to top

PUTIN 'AZITIA TUMBO JOTO' NCHI ZA MAGHARIBI

18 June 2024
Share

Rais wa Urusi Vladimir Putin anatazamiwa kuzuru Korea Kaskazini kwa ziara ya siku mbili wiki hii, nchi zote mbili zilitangaza Jumatatu baada ya miezi kadhaa ya uvumi na kukiwa na wasiwasi wa kimataifa kuhusu ushirikiano wao wa kijeshi.

Mwaka jana, kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un alisafiri hadi kituo cha Siberia cha kurusha roketi kukutana na Putin, baada ya mkutano huo, Kim alimwalika kiongozi huyo wa Urusi kutembelea Pyongyang.

Hii itakuwa safari ya kwanza ya Putin nchini Korea Kaskazini katika kipindi cha miaka 24, kwani alitembelea Pyongyang kwa mara ya kwanza Julai 2000, miezi kadhaa baada ya uchaguzi wake wa kwanza alipokutana na babake Kim, Kim Jong Il, ambaye alitawala nchi wakati huo.

Kuna wasiwasi unaoongezeka kuhusu mpango wa silaha ambapo Pyongyang inaipatia Moscow silaha zinazohitajika sana, ili kuchochea vita vya Putin nchini Ukraine badala ya usaidizi wa kiuchumi na uhamishaji wa teknolojia ambao ungeongeza tishio la silaha za nyuklia za Kim na mpango wa makombora.