
Rais wa Urusi Vladimir Putin ameamuru vikosi vya kulinda nchi yake vinavyojumuisha silaha za Nyuklia kuwa katika hali ya tahadhari ya mapigano.
.
Putin ameyasema hayo kupitia Televisheni ya Taifa ambapo amesema kuwa hatua hiyo inafuata kutokana na nchi za magharibi kuanza kuchukua hatua zisizo rafiki kwa nchi yake akimaanisha vikwazo ambavyo amesema ni haramu na matamshi ya kichokozi kutoka kwa maafisa wakuu wa nchi zinazoongoza NATO.
