Back to top

Radi yaua wanafunzi 4 wa shule ya Sekondari Nachunyu na kujeruhi 24.

27 February 2021
Share

Wanafunzi wanne wa shule ya sekondari Nachunyu wilaya ya Tandaimba mkoani Mtwara wamefaki dunia huku ishirini na nne wakijeruhiwa na radi akiwemo mwalimu kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha mkoani humo.

Kamanda wa Polisi mkoani humo Mark Njera amesema maafa hayo yametokea wakati wanafunzi hao wa kidato cha pili na cha tatu wakiwa darasani.

Amesema madarasa ya kidato cha pili na cha tatu yameungana na yapo karibu na nishati ambayo inatumika kuunganisha mtandao unaowasaidia katika masuala ya Internet na hivyo kuleta mvuatano na radi na kusababisha ajali hiyo.

Wanafunzi waliofariki dunia ni Fatuma Hassani wa kidato cha pili, Sajida Namata kidato cha tatu, Mushadi Namkoka kidato cha pili na Saumu Mdimu wa kidato cha 2.

Aidha Majeruhi 24 wamepata matibabu na afya zao zinaendelea vizuri.