Back to top

Raia 24 wa Ethiopia na Zambia mbaroni kwa kugushi nyaraka za serikali.

23 March 2020
Share

Idara ya Uhamiaji mkoani Rukwa inawashilikilia watu ishirini na wanne raia wa Ethiopia na Zambia kwa tuhuma za kugushi nyaraka za serikali na kuingia nchini bila vibali.

Kamishina Msaidizi wa Uhamiaji mkoani Rukwa Elizeus Mshongi amesema watu hao waliwakamata usiku kwenye gari ya abiria inayofaanya safari zake mkoani Njombe wakiwa na vitambulisho vya nchi ya  Ethiopia.

Wakizungumza na ITV DIGITAL kuhusu kukamatwa kwa wahamiaji hao haramu, baadhi ya wananchi mkoani Rukwa wameitaka serikali iwachukulie hatua kazi za kisheria, ikizingatiwa kwa dunia imo katika mapambano dhidi ya virusi vya Corona.