Back to top

Raia kadhaa waokolewa kiwanda cha chuma Mariupol.

02 May 2022
Share

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy amesema karibu raia 100 wa Ukraine wameondolewa kwenye kiwanda cha chuma cha Azovstal kilichozingirwa na majeshi ya Urusi mjini Mariupol nchini  Ukraine huku Wizara ya ulinzi ya Urusi ikipingana na idadi hiyo na kusema watu 80 ndio waliookolewa.

Wizara ya Ulinzi ya Urusi imeongeza kuwa waliotaka kwenda katika maeneo yanayodhibitiwa na Ukraine wamekabidhiwa maafisa wa Umoja wa Mataifa na Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu. 

Bado haijajulikana ni kwanini kumekuwa na hesabu utofauti ingawa Umoja wa Mataifa na shirika hilo la msalaba mwekundu wote hawakutoa idadi hasa ya waliokuwa wakisafirishwa. 

Taarifa kutoka chombo kimoja cha habari cha Urusi imesema idadi ya raia waliosalia katika kiwanda hicho cha chuma mjini Mariupol ni zaidi ya watu 500.