Back to top

Raia Saba wa Iran waliokamatwa na Dawa za kulevya wafikishwa mahakaman

30 April 2021
Share

Watuhumiwa saba raia wa Iran waliokamatwa na zaidi ya tani moja ya dawa za kulevya wiki iliyopita  wilayani Kilwa mkoani Lindi, wamefikishwa katika mahakama ya mkoa wa Lindi.


Watuhumiwa hao walikamatwa na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya kwa kushirikiana na  kikosi cha wana maji cha Jeshi la Wananchi  wa Tanzania, eneo la Kilwa Masoko katika bahari ya Hindi wakisafirisha dawa hizo kwa kutumia Jahazi la Al Arbo.