Back to top

Raia sita wa Ethiopia wakamatwa kwa kuingia nchini bila vibali.

22 April 2018
Share

Idara ya uhamiaji mkoa wa Mara imefanikiwa kuwakamata raia sita wa nchini Ethiopia baada ya kuingia nchini kupitia mpaka wa Sirari wilayani Tarime wakitokea nchi jirani ya Kenya katika oparesheni kali ya kupambana na wahamiaji haramu mkoani Mara.

Afisa uhamiaji mkoa wa Mara Bw. Frederick Kiondo,amesema raia wa nchi ya Ethiopia wamekamatwa maeneo ya wilaya ya Butiama wakiwa njiani kuelekea mkoani Mwanza, huku akionya baadhi ya watanzania kujihusisha na biashara hiyo haramu.

Kwa sababu hiyo afisa huyo wa idara ya uhamiaji mkoa wa Mara,amesisitiza kuchukua hatua kali katika kudhibiti biashara hiyo haramu,ikiwa ni pamoja na kutaifisha vyombo vya usafiri vinavyotumika kusafirisha na nyumba inayotumika kuwahifadhi wahamiaji hao haramu.