Back to top

RAILA ODINGA ASHINDWA KUANDAMANA KISA MAFUA

21 July 2023
Share

Baada ya watu wengi kuuliza yuko wapi Raila Odinga baada ya kutoonekana kwenye maandamano ya siku tatu mfululizo aliyoyatangaza, kwa lengo la kupinga gharama kubwa za maisha nchini Kenya, Kiongozi huyo wa Upinzani, amesema hakuwepo kwenye maandamano kwa sababu alikuwa akiumwa mafua, ambapo amesema anaendelea kupata nafuu, atakuwa sawa.
.
Odinga ameyasema hayo wakati akiongea na kituo cha Runinga cha NTV, ingawa hakusema ni wapi alipo kwa sasa, ambapo amebainisha kuwa maandamano hayo si yake na washirika wake bali ni ya Wakenya wote.