Back to top

RAIS AWAASA VIONGOZI WA DINI KULIOMBEA TAIFA

19 November 2022
Share

Rais Samia Suluhu Hassan, amewaasa viongozi wa dini nchini, waendelee kuliombea taifa lipate nafuu, kukabiliana na athari mbaya za mabadiliko ya tabia nchi.

Amezitaja athari hizo mbaya kuwa ni pamoja na ukosefu wa mvua katika baadhi ya maeneo nchini, na wawahimize waumini wa madhehebu yao wapande miti ili kulinda vyanzo vya maji na uhifadhi wa mazingira.

Akizungumza Jijini Dodoma, katika sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya Kanisa la Waadventista Wasabato pia amewataka viongozi hao wawe mabalozi wa kuielimisha jamii.

Kuhusu maadili katika jamii, amewaasa viongozi wa dini waendelee kushirikiana na serikali kukemea vitendo viovu.

Awali Mwenyekiti wa Kanisa la Waadventista Wasabato Tanzania Umoja wa Kusini, Mchungaji Dkt.Godwin Lekundayo alisema Kanisa litaendelea kushirikiana na serikali katika kuwajenga vijana kimaadili.