Back to top

"RAIS BIDEN YUKO SAWA" IKULU YA MAREKANI.

02 June 2023
Share

Ikulu ya White House nchini Marekani,  imesema Rais Joe Biden yuko sawa kiafya , licha ya kujikwaa kwenye kile kinachodaiwa kuwa mfuko wa mchanga na kuanguka , baada ya kumaliza kutoa vyeti vya Diploma katika sherehe ya kuhitimu, katika Chuo cha Jeshi la Anga la Marekani ,huko Colorado.

Rais Biden alianguka alipokuwa akielekea kwenye kiti chake,ambapo alijikwaa na kuanguka chini, kundi la wanaume, ikiwa ni pamoja na afisa wa Chuo cha Jeshi la Anga na maajenti wawili wa Huduma ya Siri, walishika mikono ya Biden kumsaidia kuinuka.

Lakini baadaye Biden alionekana vizuri  akitembea bila msaada hadi kwenye kiti chake kwenye jukwaa, ambapo baada ya sherehe kuitimishwa  alionekana akitabasamu na kukimbia kuelekea kwenye gari lake.