
Msemaji wa Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika kusini amesema kuwa Rais huyo anayekabiliwa na kashfa ya fedha zilizofichwa shambani kwake, hana nia ya kujiuzulu na kwamba ataendelea kupambana kisiasa na kwa njia za kisheria.
.
Rais Ramaphosa amekuwa akikabiliwa na kashfa hiyo tangu Juni baada ya Mkuu wa zamani wa Ujasusi, Arthur Fraser, kuwasilisha malalamiko kwa Polisi akimshtumu Rais huyo kwa wizi wa zaidi ya Tsh. Bil.9 zilizokuwa katika shamba lake mwaka 2020.
