Back to top

Rais Dkt.Magufuli atengua tamko la wizara ya elimu.

14 December 2018
Share

Rais Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli amefuta maelekezo ya wizara ya elimu kwenda kwa wakuu wa vyuo vya ualimu, wakuu wa vyuo vya maendeleo ya jamii, wakuu wa vyuo vikuu na vyuo vikuu vishiriki na taasisi zilizochini ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia la kutaka rangi ya njano kwenye bendera ya taifa itambulike kama rangi ya dhahabu.

Mhe. Rais Magufuli amesema maelekezo hayo yanaathiri uzalendo wa Watanzania na yanaleta mkanganyiko wa tafsiri ya rangi na alama zilizomo katika bendera ya Taifa.
“Hata mimi mwenyewe tangu nasoma shule hadi leo nafahamu kuwa Bendera ya Taifa ina rangi ya njano na sio rangi ya dhahabu, na rangi hiyo ya njano inawakilisha madini yote, sio dhahabu pekee yake. Kwa hiyo nimeamua kuifuta barua hiyo na kama kuna mabadiliko basi ni lazima yafanyike kwa kuzingatia taratibu zote kwa kuwa jambo hili ni la Kitaifa, sio la mtu mmoja” amesisitiza Mhe. Rais Magufuli.