Back to top

RAIS DKT.SAMIA AWAPA KONGOLE MABALOZI

22 April 2024
Share

Rais wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amewapongeza Mabalozi wanaowakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali duniani, kwa kazi nzuri ya uwakilishi ambayo inaonekana kwa kuongezeka kwa masoko ya bidhaa za Tanzania, biashara, uwekezaji, utalii na tekbolojia nchini.

Mhe.Rais Samia ametoa pongezi hizo leo alipokuwa anawahutubia Mabalozi hao kwa njia ya mtandao ambao wamekusanyika mjini Kibaha kwa warsha ya siku 4 ya kutathimini utekelezaji wa Sera ya Mambo ya Nje iliyoanza Aprili 21 na itakamilika Aprili 24, 2024.

Mhe. Rais Samia amesema kuwa nchi inawategemea sana Mabalozi katika utekelezaji wa majukumu yao ili iweze kusonga mbele kiuchumi na kwa kuliona hilo, Rais Samia amesema amechukua hatua mbalimbali ili kuibadilisha Wizara ya Mambo ya Nje iwe ya kisasa zaidi na kuwa na uwezo wa kuitangaza nchi.

Lengo la Mabadiliko hayo ni kuifanya nchi iendelee kuheshimika na kuwa na ushawishi zaidi duniani kama ilivyokuwa katika miaka ya nyuma ya wakati wa harakati za ukombozi na baada ya ukombozi.