Back to top

RAIS DKT.SAMIA KUZINDUA UJENZI BANDARI YA KILWA

14 September 2023
Share

Rais wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuzindua ujenzi wa Bandari ya Uvuvi ya Kilwa Masoko Septemba 19, 2023, ambayo haijawahi kuwepo tangu nchi ipate uhuru, ambapo uzinduzi huo utaweka historia katika sekta ya uvuvi.  

Akiongea na waandishi hao wa habari, Waziri Ulega amesema hatua hiyo ya Rais, Dkt.Samia ya kuzindua ujenzi wa bandari hiyo ni ishara kwamba anakwenda kuandika historia mpya na kitendo hicho kinaonesha dhamira yake ya dhati ya kuleta mapinduzi ya kiuchumi kupitia sekta ya uvuvi hapa nchini.

Hayo yamefahamika wakati Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuhusu ziara ya Mheshimiwa Rais, Dkt.Samia Suluhu Hassan ya uwekaji wa jiwe la msingi la mradi wa bandari ya uvuvi ya Kilwa na ugawaji wa boti za kisasa za Uvuvi, Wilayani Kilwa, Mkoani Lindi leo Septemba 14, 2023.

Amesema ujenzi huo wa bandari ukikamilika Watanzania takribani Milioni 5, watapata kipato chao kutokana na shughuli za uvuvi na zinazohusiana, ikiwemo pamoja utengenezaji wa boti, ukarabati wa nyavu, usindikaji wa samaki, na biashara mbalimbali ndogondogo.

Ameongeza kuwa ujenzi wa bandari hiyo unaashiria mwanzo wa enzi mpya za uvuvi wa kisasa Tanzania ambapo wakazi wa maeneo ya Pwani watapata ajira zaidi ya 30,000, fursa mpya za biashara na pia tekinolojia mpya.

Waziri Ulega amesema uzinduzi wa bandari hiyo itakuwa ni mkombozi kwa sekta ya uvuvi kwani itawezesha Tanzania kuwa na nafasi kubwa katika soko la Kimataifa la Uvuvi, kuongeza fursa za ajira kwa Watanzania na pia kuleta tija kwa wavuvi wadogo na wakubwa.

Kuhusu ugawaji wa boti za Uvuvi, Waziri Ulega alisema kufuatia mpango wa Wizara wa kutoa mkopo wa masharti nafuu wa Boti za kisasa za Uvuvi na vifaa vyake, unalenga kubadilisha maisha ya wavuvi, kutoa ajira nyingi zaidi, na kukuza uchumi wa Tanzania