Back to top

Rais Filipe Nyusi wa Msumbiji kutua nchini kwa ziara ya siku mbili.

10 January 2021
Share

Rais wa Msumbiji Felipe Nyusi anatarajiwa kufanya ziara ya kikazi ya siku mbili nchini kuanzia Januari 11, 2020.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof.Palamagamba Kabudi amesema kuwa, Rais Nyusi alipanga kufanya ziara nchini tangu mwaka 2020, lakini kutokana na ratiba ya Uchaguzi Mkuu hapa nchini, alisogeza mbele ziara hiyo.

Kabudi ametoa taarifa ujio wa Rais Nyusi nchini wakati akizungumza na Wanahabari mkoani Geita.

"Ni dhahiri kabisa katika ziara hii, haiwezekani ndugu yetu wa damu Rais kutoka Msumbiji aje asikutane na wananchi na asifanye shughuli na wananchi, ratiba inaandaliwa ya yeye kukutana na wananchi hapa Chato na kufanya shughuli hapa Chato"-Prof.Kabudi.

Kabudi amesema kuwa Mahusiano ya Tanzania na Msumbiji ambayo ni ya Kihistoria na Kidiplomasia yameendelea kuimarika, Uhusiano wa Kiumchumi nao umeendelea kuimarika.

Kabudi ameongeza kuwa katika ujio wa Rais Nyusi ataacha kumbukumbu kwa Watanzania na wana Chato kwani atakuwa na shughuli zingine nje licha ya kukutana na mwenyeji wake.