Back to top

Rais Hichilema asafiri kwa ndege ya abiria.

20 September 2021
Share

Kuelekea kufanyika kwa mkutano wa Umoja wa Mataifa(UN) nchini Marekani, Rais wa Zambia, Haikainde Hichilema amesafiri kwa ndege ya abiria huku akipanda daraja la chini kabisa na akisindikizwa na maafisa watatu tu.
.
Rais Hichilema amesema gharama zitakazookolewa kwenye safari hiyo zitatumika kupambana na umasikini, na amewahakikishia wananchi wake kuwa mijadala yote kwenye mkutano huo itakuwa ya kuwanufaisha Wazambia.