Rais wa Tanzania Mh.John Pombe Magufuli ameagiza wakala wa Barabara TANROAD na wakala wa Barabara vijiji TARURA kuanza maramoja ujenzi kwa kiwango cha lami barabara ya kutoka Kilolo hadi Iringa yenye urefu wa kilomita 35 ili kuondoa kero ya ubovu miundombinu wilayani humo.
Rais Magufuli ametoa agizo hilo baada ya kuweke jiwe la msingi la ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Kilolo utakao gharimu zaidi ya shilingi Bilioni 4.
Akizungumza na wananchi hao kwenye mkutano wa hadhara Rais Magufuli pia ameagiza halmashauri zote nchini kutenga mfuko maalumu wa dawa ili kuimarisha upatikanaji wa dawa kwenye hospitali za wilaya.
Kwapande wake Waziri wa TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo amesema serikali imetenga zaidi ya Shilingi Bilioni 105 kwaajili ya kujenga hospitali mpya 67.
Naye Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Wiliam Lukuvi amekeme uuzaji holela wa ardhi wilayani Kilolo huku Mkurugenzi wa halamshauri ya wilaya ya Kilolo Bwana. Aloys Kwezi akibainisha kuwa ujenzi wa hospitali hiyo unalega kuondoa kero ya upatikanaji wa huduma za afya wilayani humo.