Back to top

Rais Magufuli amsamehe Kaimu DED  Rufiji aliyemdanganya.

12 August 2020
Share

Rais wa Jamhuri ya Muungano  wa Tanzania Dk John Magufuli amemsamehe Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri  ya wilaya ya Rufiji Brighton Eliud Kilimba aliyetoa  taarifa  za uongo juu ya ubovu wa gari la kubebea  wagonjwa kituo cha afya Ikwiriri Rufiji na sasa yupo  huru licha ya taratibu za kumfikisha mahakamani kuwa zilikwishakamilika. 

Kamanda wa polisi mkoa  wa Kipolisi Rufiji Kamishna Msaidizi Onesmo Lyanga  amethibitisha kutolewa  kwa msamaha huo kutoka  kwa. Mh  rais .
 
Mapema Julai 30 mwaka huu majira ya saa 9 mchana Rais Magufuli akitokea  kijijini Lupaso wilayani Masasi mkoani Mtwara katika maziko ya aliyekuwa  rais wa awamu ya tatu aliposimama Ikwiriri Rufiji mkoani Pwani kusikikiza  kero mbalimbali inadaiwa Bw. Kilimba  alitoa  taarifa  za uongo  kwa Mhe  rais kuwa  gari  la kubebea wagonjwa ni bovu  liko gereji na linahitaji gharama kubwa za matengenezo  wakati  anajua sio kweli.