Back to top

Rais Magufuli amuapisha Bashiru kuwa Balozi na Katibu Kiongozi.

27 February 2021
Share


Rais Dkt.John Magufuli amemuapisha Bashiru Ali Kakurwa kuwa Katibu Mkuu Kiongozi katika hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.

Kabla ya kuteuliwa Februari 26,2021 kuwa Katibu Mkuu Kiongozi kuchukua nafasi ya Marehemu Balozi John Kijazi aliyefariki dunia  Februari 17,2021, Dkt.Bashiru Ali Kakurwa alikuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi.

Akizungumza baada ya kuapishwa, Balozi Bashiru amemshuru Rais kwa kumteua, kuitumika nafasi hiyo kwa uadilifu na kuomba shirikiano  kutoka kwa watendaji wengine wa serikali na mihimili mingine ya dola, ili kufanikisha utekelezaji wa majukumu ya serikali.

Kwa upande wao, Naibu Spika Dkt.Tulia Ackson na Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma ambao ni viongozi wakuu wa mihimili mingine ya dola yaani Bunge na Mahakama, wameahidi kumpa ushirikiano, ili afanikishe utekelezaji wa majukumu yake.

Hafla hiyo, pia ilihudhuriwa na Makamu wa Rais Mhe.Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa.