Back to top

Rais Magufuli ateua DC Mvomero na DED Biharamulo.

05 July 2020
Share

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 05 Julai, 2020 amemteua Bw. Albinus Mgonya kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro.

Kabla ya uteuzi huo, Bw. Mgonya alikuwa Katibu Tawala Msaidizi Mkoa wa Rukwa na anachukua nafasi ya Bw. Mohamed Musa Utaly.


Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. Waziri Khachi Kombo kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo Mkoani Kagera.

Kabla ya uteuzi huo, Bw. Kombo alikuwa Afisa Utumishi wa Manispaa ya Morogoro na amechukua nafasi ya Bi. Wendi Ng’ahala Uteuzi wa viongozi hao umeanza leo tarehe 05 Julai, 2020 na wateule wote wanatakiwa kuwepo Ikulu, Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 06 Julai, 2020 saa 4:00 asubuhi.