Back to top

Rais Magufuli awabadili vituo vya kazi Wakuu wa Wilaya .

13 August 2020
Share

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amefanya mabadiliko ya vituo vya kazi kwa Wakuu wa Wilaya 2 kama ifuatavyo;

Kwanza, Mhe. Rais Magufuli amemhamisha kituo cha kazi aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Rorya Mkoani Mara Bw. Simon Kemori Chacha, kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Chemba Mkoani Dodoma.

Pili, Mhe. Rais Magufuli amemhamisha kituo cha kazi aliyekuwa Mkuu wa Wilaya Chemba Mkoani Dodoma Bw. Simon Ezekiel Odunga, kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Rorya Mkoani Mara.

Mabadiliko ya vituo vya kazi kwa Wakuu wa Wilaya hao yanaanza leo tarehe 13 Agosti, 2020.